Beki wa kati wa Yanga Ladslaus Mbogo aliyechana kiatu cha
mshambuliaji Jerry Tegete kutokana na daruga lake, amesema yake ya moyoni.
Mbogo maarufu kama Mnyama kutokana na uchezaji wake wa kutumia
nguvu au kutotaka mchezo hata mazoezini, amesema kiatu cha Tegete kimetengenezwa
China.
Salehjembe iliamua kumsaka Mbogo ili aelezee namna
alivyochana kiatu cha Tegete wakati wakiwa mazoezini juzi, hali iliyowashangaza
wengi waliokuwa kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mbogo (kulia) na Tegete...
Lakini yeye alisisitiza ilikuwa ni mchezo wa kawaida tu
lakini kwa kuwa kiatu cha Tegete kimetengenezwa India, ilikuwa lahisi
kuchanika.
“Aah, ilikuwa kawaida tu, sema huyu alikuwa amevaa kiatu
kilichotengenezwa India,” alisema Mbogo mbele ya Tegete.
Tegete naye alijibu: “Usipoangalia huyu jamaa anaweza kukua,
ni hatari sana. Kama kiatu kinachanika vile, binadamu itakuwaje.”
Tegete aliendelea kusisitiza huwa havai viatu feki lakini
kazi ya Mbogo ni zaidi ile ya jeshi, hivyo akamuomba Mbogo apunguze madaruga
kama ambavyo Kocha Ernie Brandts amekuwa akiomba.
Mbogo amesajiliwa na Yanga akitokea Toto African, ingawa
hajapata namba kutokana na Yanga kuwa na mabeki wengi zaidi wenye uwezo, lakini
ni kati ya wachezaji wazuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment