March 7, 2013




Osiah..
Baada ya mzozo wa karibu wiki mbili kati ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na serikali, hatimaye pande hizo mbili zilikutana leo.

Mkutano huo uliofanyika katika Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo uliongozwa na Naibu Waziri, Amos Makalla ambaye awali TFF ilitangaza kutaka asihudhurie kwa kuwa hawana imani naye kuhusiana na suala la katiba yao ya mwaka 2006 kukataliwa.


Hata hivyo hiyo jana, Makalla pamoja na katibu mkuu wa wizara hiyo ndiyo waliongoza kikao hicho.
Makalla hakutaka kuweka wazi kilichozungumziwa licha ya kukubali kwamba kweli walikutana. Badala yake akasema kuna maagizo wameyatoa.
 Makalla...
“Kuna maagizo yanatakiwa yatekelezwe, tumeshazungumza nao,” alisema kwa ufupi.
Kwa upande wa TFF, Katibu Mkuu, Angetile Osiah alikubali kuwa walikutana lakini akasisitiza kazi ya kulizungumzia hilo ni ya wizara ambao walikuwa wenyeji.
Awali Osiah alieleza wazi wao kutokuwa na imani na Makalla ambaye baadaye alisisitiza kwamba katibu huyo ndiye mwenye matatizo.

Huenda kesho asubuhi ufafanuzi zaidi kuhusiana na kilichofikiwa katika kikao hicho, kikawekwa wazi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic