March 4, 2013


Bondia maarufu wa  ngumi za  kulipwa  nchini, Mchumia Tumbo amefanikiwa..



Marwa dhidi ya Mchumiatumbo....ilikuwa ni ngumi mawe..


Kaseba...JUU, akimchakaza Mtambo wa gongo, CHINI, akipongezwa na Dotnata
Mkongwe Joseph Marwa aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda pambano lake la uzito wa juu dhidi ya Alphonce Mchumiatumbo, alijikuta akishindwa kuvumilia makonde zaidi katika raundi ya sita.

Marwa alichapwa makonde mfululizo na kuanguka, hali iliyomfanya ashindwe kuendelea.

Wakati pambano jingine, Japhet Kaseba alifanikiwa kumshinda mkongwe Maneno Oswald ‘Mtambo wa gongo’ kwa pointi katika pambano lililokuwa na ushindani mkali.

Mapambano yote yalifanyika kwenye Ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic