March 3, 2013



Baada ya kucheza mechi yake ya 28 msimu huu dhidi ya Norwich, wababe Man United wamefikisha mechi 800 za Ligi Kuu England.
Rekodi hiyo ya Man United inaunganishwa na timu nyingine zilizokuwa katika ligi hiyo kuanzia msimu wa 1992-93 bila kuteremka daraja.

Katika mechi hizo 800, Man United imeonyesha imekuwa na kikosi imara kwa muda mrefu, kwani pamoja na kushinda mataji 12, lakini imefanikiwa kushinda mechi 522 ambayo ni karibu ya robo tatu ya mechi zake.

Imeshinda mataji hayo 12 ndani ya misimu 20 na kocha wake, Alex Ferguson ndiye kocha aliyekuwa kwenye ligi hiyo tokea msimu huo na kuiongoza timu yake kushinda mabao 1,605 huku akiwa na beki iliyofungwa mabao 691 tu.

Arsenal imekuwa ya pili, ikiwa imeshinda ubingwa mara tatu chini ya Wenger, Chelsea ya tatu ikiwa na vikombe kibao ingawa vitatu ndiyo vya Premiership.
Liverpool inashika nafasi ya nne ikiwa chini ya Chelsea na Arsenal ingawa kihistoria inaonekana ni klabu kubwa zaidi. Nyingine zenye mafanikio zaidi ni Tottenham Hotspur, Aston Villa na Everton.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic