Beki mpya wa kati wa Yanga, Ladslaus Mbogo amepewa jina la
Myama na wachezaji wenzake. Anajulikana kuwa hataki mchezo mazoezini.
Mnyama hataki mchezo kweli, kwani hata mazoezini yeye
anacheza kama yuko katika mechi na kama anakwenda kukaba, basi kila mmoja
anahisi ni hatari.
Mara nyingi Kocha Mkuu, Ernie Brandts amekuwa akilazimika
kusimamisha mazoezi na kumkumbusha beki huyo wa zamani wa Toto African kwamba
apunguze nguvu ili asiwaadhibu zaidi wachezaji wenzake.
Kudhihirisha hilo, katika mazoezi ya jana ya Yanga, Mbogo
alichana kiatu aina ya Adidas cha mshambuliaji Jerry Tegete.
Tegete alikutana na daruga la Mbogo na kuchana kiatu hicho. Tayari
Tegete ameamua kununua kiatu kingine huku akisema Mbogo ni hatari sana.
“Kweli jamaa muacha aitwe Mnyama, angalia kiatu change. Jamaa
kakimaliza kabisa, inabidi ninunue kingine,” alisema Tegete.
Juhudi za kumpata Mnayama ili azungumzie hilo bado
zinaendelea ili kujua kweli kama ni mazoezi tu anachana hadi viatu, siku
akipewa mechi, si ataua huyu?
0 COMMENTS:
Post a Comment