Nyota wa Barcelona, Lionel Messi ameweka
rekodi nyingine ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao 19 ndani ya miezi mitano.
Lakini rekodi hiyo mpya inaboreshwa
na Messi kufunga bao dhidi ya kila timu ya La Liga ambayo imekutana na Barcelona
katika ligi hiyo.
Wakati Barcelona ilitoka sare ya
mabao 2-2 dhidi ya Celta Vigo, Messi alifikisha mabao 43 ya La Liga na mechi
nane tu zimabaki kabla ya kufikia mwisho wa msimu.
Messi amefunga mabao 30 katika mechi
19 za La Liga. Picha hiyo ya graphics hapo chini inaonyesha namna Messi
alivyofunga mabao katika mechi hizo za La Liga.
Kwa sasa, Messi raia wa Argentina ndiye
mchezaji maarufu zaidi, hatari zaidi na mwenye uwezo mkubwa zaidi kuliko
mwingine yoyote.
0 COMMENTS:
Post a Comment