March 3, 2013



ALBA: SIKUNYOOSHA KIDOLE NITUKANE, NILIMAANISHA MESSI NAMBA ONE
 Beki wa kushoto wa Barcelona, Jordi Alba ameingia matatani baada ya kunyoosha kidole cha kati kwa mashabiki wa Real Madrid wakati akishangilia bao la kusawazisha lililofungwa na Lionel Messi.

Alba alionekana akinyoosha kidole cha kati ikiwa ni ishara ya kuwatusi mashabiki wa Madrid waliokuwa kimya kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Santiago Bernabeu, jana.
Lakini Alba amesema alichomaanisha ni mfungaji wa bao hilo, Lionel Messi ni mchezaji namba moja na wala hakuwa akitukana.




 PIQUE ATAKA MWAMUZI AOMBE RADHI HARAKA
Beki wa kati wa Barca, Gerard Piqué amemshambulia mwamuzi wa mchezo wa El Clasico uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Pique amesema mwamuzi, Pérez Lasa anapaswa kuomba radhi kwa wadau wa soka wa Hispania na mashabiki wa Barcelona kutokana na kiwango kibovu alichoonyesha.

“Kweli hatukuwa katika hali nzuri, lakini baadaye tulibadilika na tulikuwa na uwezo mkubwa wa kushinda, lakini mwamuzi ndiyo akawa tatizo kwetu. Kama vile alikuwa na matokeo yake, anapaswa kuomba radhi,” alisema.


MESSI AFIKISHA MABAO 18 EL CLASICO
Pamoja na Barcelona kupoteza mechi dhidi ya wapinzani wao wakubwa Real Madrid, Lionel Messi maarufu kama Leo amefanikiwa kufikisha mabao 18 aliyofunga katika mechi za El Clasico.

Kwa kufikisha mabao 18 katika mechi zilizozikutanisha Real Madrid na Barca, Messi amelingana na mshambuliaji nyota wa zamani wa Real Madrid, Alfred di Stefano aliyeongoza kwa muda mrefu.

Kabla ya mechi ya jana, Messi alikuwa na mabao 17, sasa amefikisha idadi sawa na Di Stefano ambaye pia ni raia wa Argentina. Raul aliyekuwa zamani Madrid, anashika nafasi ya tatu kwa kuwa na mabao 15.

RONALDO AMPIGA BAO MESSI, AMUALIKA MARADONA ASHUHUDIE BARCA IKIUWAWA
Mshambuliaji nyota wa zamani wa Argentina, Diego Armando Maradona alikuwa mmoja wa watazamaji waliokuwa uwanjani wakati Real Madrid ilipokuwa ikipambana na wapinzani wake Barcelona katika mechi ya La Liga, jana.

Maradona alionekana akiwa katika sehemu maalum, maarufu kama Box inayomilikiwa na Ronaldo akishuhudia mechi hiyo.

Hali hiyo imeonyesha kuwashangaza wengi kwa kuwa walitegemea Maradona angealikwa na Messi, Muargentina mwenzake ambaye amekuwa akimtetea kila kukicha lakini pia aliwahi kuwa kocha wake wakati wa Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010.

ACTION....


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic