Nakukumbusha, hii ndiyo Pamba ya Mwanza enzi hizo, timu yenye uwezo
mkubwa na wachezaji ambao kama leo wangekuwa wanacheza, basi Ulaya ni kunusa tu.
Waliocheza Simba enzi hizo waulize kikosi hiki, TP Lindanda au Wana
Kawekamo.
Waliosimama toka kushoto: Madatta Lubigisa, Rajabu Musoma, Beya Simba,
Nteze John ‘Lungu’, Kitwana Selemani ‘Popat’, Fumo Felician, Pascal Mayala na
Paul Rwechungura.
Waliokaa toka kushoto: George Gole, Khalfan Ngassa, Ally Bushiri,
Alphonse Modest, Mao Mkamy ‘Ball Dancer’, Saleh Muhammad, Hamisi Nyembo na Nico
Bambaga
Kilichofuata baada ya hapo: Madatta alistaafu akiwa Pamba, Beya na Nteze
walitua Simba, Fumo na Mayala walienda Yanga, Gole alibaki Pamba, Ngassa na
Ball Dancer walitua Simba, Modest alienda Simba kisha Mtibwa Sugar, Bambaga alienda
Malindi kisha Simba.








0 COMMENTS:
Post a Comment