Ushindi wa
mabao 3-1 dhidi ya African Lyon, umeipa Azam F nafasi kubwa ya kuendelea kuipa
presha Yanga.
Kwa ushindi
huo, Azam FC imefikisha pointi 46, huku Yanga iliyo kileleni ikiwa na 49.
Katika
mechi hiyo ya leo kwenye Uwanja wa Chamazi Complex nje ya jiji la Dar es
Salaam, Azam ilionyesha imepania kushinda tokea mwanzo.
Bao lake la
kwanza lilipatikana mapema tu katika dakika ya tisa kupitia kwa Hamis Mcha ‘Vialli’
na Kipre Tchetche akaongeza la pili katika dakika ya 28.
Pamoja na
kwanza Azam FC walikuwa wanashambulia mfululizo lakini Lyon walikuwa wakijibu
mashambulizi na katika dakika ya 28, Adam Kingwande alifunga bao zuri kwa shuti
kali na kufanya timu hizo ziende mapumziko matokeo yakiwa 2-1.
Kipindi cha
pili kilikuwa ni vuta nikuvute lakini Tchetche tena ambaye dalili zinaonyesha
ndiye atakuwa mfungaji bora, alifunga bao la tatu na la pili kwake katika
dakika ya 61.
Kutokana na
mambo yanavyokwenda, maana yake Azam FC inaipa presha kubwa Yanga katika mechi
yake ya kesho dhidi ya Oljoro kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
KIKOSI AZAM:
1. Aishi Salum
2. Himidi Mao
3. Waziri Salum
4. Jockins Atudo
5. Luckson Kakolaki
6. Jabir Aziz
7. Kipre tchetche
8. Ibrahim Mwaipopo
9. Abdi Kassim
10. Salum Abubakar (C)
11. Mcha Khamisi
Akiba
Mwadini Ali
Humphrey Mieno
Seif Karihe
Malika Ndeule
Gaudence Mwaikimba
Omari Mtaki
Brian Umony
KIKOSI AZAM:
1. Aishi Salum
2. Himidi Mao
3. Waziri Salum
4. Jockins Atudo
5. Luckson Kakolaki
6. Jabir Aziz
7. Kipre tchetche
8. Ibrahim Mwaipopo
9. Abdi Kassim
10. Salum Abubakar (C)
11. Mcha Khamisi
Akiba
Mwadini Ali
Humphrey Mieno
Seif Karihe
Malika Ndeule
Gaudence Mwaikimba
Omari Mtaki
Brian Umony
0 COMMENTS:
Post a Comment