April 11, 2013




Vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga itashuka uwanjani kuivaa JKT Oljoro bila ya beki wake kisiki wa kulia, Mbuyu Twite.

Twite anakaa benchi kutokana na kuwa na kadi tatu za njano, kadi ya mwisho aliipata wakati timu hiyo ilipoivaa Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.


Habari za uhakika ambazo Salehjembe imezipata ni kwamba tayari Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amemtayarisha Juma Abdul katika nafasi hiyo ya beki wa kulia.

Kawaida Mholanzi huyo, amekuwa akimuamini zaidi Twite raia wa Rwanda mwenye asili ya DR Congo katika nafasi hiyo ya kulia.

Wiki iliyopita, Brandts alilaumu kuhusiana na kadi aliyopewa Twite katika mechi hiyo dhidi ya Polisi kwa madai kuwa beki huyo alisukumwa na ndiye aliyepewa kadi.

Abdul ambaye amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Mtibwa Sugar, ameshindwa kupata namba ya kudumu Yanga, ingawa ndiye chaguo la pili la kocha huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic