Mshambuliaji
wa Yanga, Jerry Tegete anatarajia kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mechi tatu za
timu hiyo ambazo ni muhimu zaidi.
Yanga ina
mechi tatu muhimu ikiwemo ya kesho dhidi ya JKT Oljoro ambazo inatakiwa
kushinda ili kutangaza ubingwa.
Kwa kuwa kila mechi ni dakika 90, iwapo Tegete atakosa mechi tatu maana yake atapoteza dakika 240 akiwa nje ya uwanja na Yanga ikipambana kupata ubingwa.
Tegete
ambaye ni mmoja wa washambuliaji tegemeo wa Yanga, huenda akazikosa mechi zote
kutokana na kusumbuliwa na maumivu makali ya goti.
Kocha Mkuu wa
Yanga, Ernie Brandts amesema amelazimika kumpumzisha Tegete kwa muda ili
kuangalia afya yake na hasa goti.
“Kutokana
na ushauri wa daktari na nilivyoiona hali halisi, Tegete analazimika kupumzika.
Ninaamini mechi tatu sidhani kama atacheza.
“Lakini
kunaweza kukaw ana mabadiliko akarudi kucheza, hivyo ni suala la kusubiri na
kumuombea apone haraka,” alisema Brandts, beki wa zamani wa timu ya taifa ya
Uholanzi.
Kwa zaidi
ya siku nne au tano, Tegete amekuwa akionekana katika mazoezi ya Yanga lakini
akiwa na nguo za nyumbani.
Mshambuliaji
huyo alianza kurudisha makali yake katika kupachika mabao lakini suala la
majeruhi limeonyesha kumrudisha nyuma.
0 COMMENTS:
Post a Comment