April 25, 2013


Jorge Messi

Wakala maarufu wa kuuza wachezaji, Josep María Minguella amesema baba yake Messi alimueleza kwamba mwanaye hakuwa fiti kucheza mechi dhidi ya Bayern Munich.

Wakala huyo amesema Jorge Messi alimueleza kwamba Messi hakuwa katika hali nzuri ya kucheza mechi hiyo lakini Barcelona walikuwa hawana namna.

“Sijasema mimi kwamba Messi hakuwa fiti kucheza, baba yake alizungumza nami na kunieleza kuhusiana na hilo.

“Lakini inawezekana kocha akawa anajua zaidi, ila baba yake pia aliwasiliana naye, hivyo anajua,” alisema.

Katika mechi hiyo ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern iliicharaza Barcelona kwa mabao 4-0 kama imesimama huku Messi akishindwa kuonyesha cheche kama ilivyozoeleka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic