April 25, 2013




Muda mchache baada ya kuiangamiza Real Madrid kwa kufunga mabao manne, mshambuliaji wa Borussia Dortmund,  Robert Lewandowski amekuwa ‘almasi’.

Klabu za Bayern Munich na Manchester United wameanza kupita kila kona kuhakikisha wanamnasa.


Mabao manne aliyofunga dhidi ya Real Madrid, yamemfanya aweke rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuifunga timu hiyo ya Hispania mabao manne katika mechi ya ligi ya mabingwa.

Manchester wangekuwa wa kwanza kumpata mshambuliaji huyo lakini Alex Ferguson akata kuwe na subira.

Lakini inaonekana Bayern ambao wameshabeba ubingwa wa Ujerumani kama ilivyo kwa Man United England, ndiyo wenye nafasi ya kumnasa.

Huenda mshambuliaji huyo raia wa Poland akachagua kubaki Ujerumani lakini akihama kutoka mji wa Dortmund hadi Munich.

Iwapo Lewandowski atakubali kujiunga timu kati ya hizo, atakuwa amebadili rangi ya jezi kutoka njano na nyeusi hadi nyekundu na nyeupe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic