Beki wa kati wa Barcelona, Gerard Piqué amelazimika kubaki mjini Munich baada ya timu yake kuchapwa mabao 3-0 na wenyeji wao Bayern Munich.
Pique amebaki mjini humo kwa siku moja zaidi ili kufanyiwa vipimo kama anatumia dawa za kuongeza nguvu.
Taarifa
zinaeleza vipimo hivyo vilifanyika juzi usiku na jana mchana, Pique aliondoka
kurejea Hispania kuungana na timu yake.
Kumekuwa na
utaratibu wa kuchagua wachezaji ambao wanapimwa kama wanatumia madawa ya
kuongeza nguvu au la na yoyote anaweza kuchaguliwa kutoka kwenye timu moja au
nyingine.
Katika
mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa, Barcelona ilichapwa kwa mabao 4-0 na inalazimika
kwenda kushinda 5-0 ili kusonga mbele.








0 COMMENTS:
Post a Comment