Gareth
Bale ameonyesha hazuiliki baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo zote mbili za
mchezaji bora wa mwaka wa England na ile ya mchezaji bora zaidi kijana zote
maarufu kama PFA.
Kiungo
huyo mwenye kasi wa Tottenham Hotspur ,23, ametwaa tuzo zote na kuingia kwenye
rekodi ya kuzibeba zote kwa wakati mmoja kama alivyofanya Andy Gray mwaka 1976-77
na Cristiano Ronaldo, miaka sita iliyopita.
Wengine
waliowahi kubeba tuzo hiyo mara mbili kwa nyakati tofauti ni Mark Hughes, Alan
Shearer, Thierry Henry na Ronaldo. Kwani aliwahi kuichukua kwa mara ya kwanza mwaka
2010-11.
Wapinzani wakubwa wa Bale katika tuzo hiyo (si ya vijana)
walionekana kuwa Robin van Persie wa Man United na Luis Suarez wa Liverpool
ambaye mwisho alionekana kujiondoa baada ya kuingia katika kashfa ya kung’ata
beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic.
Akizungumzia tuzo hizo, Bale alisema: “Ni kitu kizuri na cha
kujivunia, kuchaguliwa na wachezaji wenzako ambao wakati mwingine ni wapinzani
wako. Hakika ni kitu cha kujivunia kwangu.
“Ukiangalia
katika majina makubwa yaliyofanikiwa kutwaa tuzo hii, unajiuliza mara mbili. Lakini
nisingefanikiwa bila ya ushirikiano wa wachezaji wenzangu pamoja na kocha
wangu, nawapa tuzo hizi kama zawadi.
“Washiriki
wengine ambao hawakupata, pia walifanya kazi nzuri sana katika klabu zao na
hawapaswi kujisikia vibaya kutokana na kukosa tuzo hii.”
Bale,
tegemeo kubwa la Spurs, amefunga mabao 19 katika mechi 29 za Ligi Kuu England
msimu huu, moja ya mabao yake yaliipa ushindi Tottehnam kwenye Uwanja wa Old
Trafford unaomilikiwa na Man United, awali haikuwa imewahi kushinda uwanjani
hapo kwa miaka 23 iliyopita.
Pamoja na Bale, PFA walichagua kikosi bora cha msimu ambacho
kilipangwa kama ifuatavyo. Kipa, De Gea (Man United), Zabaleta (Man City),
Baines (Everton), Ferdinand (Man United), Vertonghen (Spurs), Carrick (Man United),
Hazard (Chelsea), Mata (Chelsea), Suarez (Liverpool), van Persie (Man United)
na Bale (Spurs).
0 COMMENTS:
Post a Comment