Na Saleh Ally
MSHAMBULIAJI
Mtanzania, Yona Ndabila ameula baada ya timu kongwe ya nchini Nepal ya Manang
FC kumsajili.
Awali
Ndabila alikuwa anakipiga katika timu ya Saraswati Youth Club ya nchini humo na
akamaliza msimu akiwa wa pili katika upachikaji mabao.
Akizungumza
na gazeti hili, Ndabila ambaye yuko nchini kwa mapumziko alisema amesaini
mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo.
“Kwangu ni
faraja kwa kuwa timu hiyo ni kati ya mbili kubwa nchini Nepal, nimekwenda
kutafuta mafanikio hivyo ninajisikia vizuri.
“Lakini
ninaona nina deni ambalo liko mbele yangu lakini nitajituma kuhakikisha
ninapata mafanikio zaidi,” alisema Ndabila.
Tayari
Ndabila ameondoka nchini kurejea Nepal kwa ajili ya kujifua na kikosi chake
hicho kipya.
Lakini
Mtanzania mwingine, kiungo wa zamani wa Yanga, Godfrey Bonny naye anarejea
katika timu yake ya Saraswati Youth Club.
Ndabila
alianza kuchipukia kisoka mkoani Mbeya na alifanya vizuri akiwa na Prisons ya
mjini humo na baadaye Mtibwa Sugar.
Wakati
akiwa nchini aliwahi kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa Stars, Marcio
Maximo lakini hakudumu muda mrefu.
0 COMMENTS:
Post a Comment