Mashabiki
na uongozi wa Queens Park Rangers umeonyesha kukasirishwa na kitendo cha beki, Jose
Bosingwa kuonekana akicheka dakika chache baada ya timu hiyo kuteremka daraja.
Wachezaji
na wadau wa QPR wamechukizwa na kitendo kinachomaanisha Bosingwa hakuumizwa
hata kidogo na wao kuteremka daraja.
Picha
zinamuonyesha beki huyo mwenye miaka 30 anayelipwa pauni 65,000 kwa wiki
akicheka wakati anaingia vyumbani mara baada ya mchezo dhidi ya Reading ambao
ulimalizika kwa sare ya bila kufungana na kuidhinisha timu zote mbili kuteremka
daraja.
Mashabiki
wa QPR wameweka picha za Bosingwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter akicheka
kama ilivyokuwa kwa mchezaji mwingine, Clint Hill.








0 COMMENTS:
Post a Comment