Dortmund ndiyo walikuwa wa kwanza
kupata bao katika dakika ya 8 kupitia kwa Lewandowski
raia wa Poland ambaye alitumia uzembe wa beki Pepe.
Lakini Madrid wakasawazisha katika dakika ya 43 mfungaji
akiwa Ronaldo baada ya kuunganisha krosi ya Higuain aliyekuwa ameungana katika
counter attack.
Baada ya hapo, Wajeurumani hao pamoja na kushangiliwa kwa
nguvu na mashabiki wao walionekana kama wamechanganyikiwa na kutoa nafasi kwa
Madrid kuanza kushambulia mfululizo.
Iwapo Madrid wangekuwa makini katika dakika tatu za mwisho,
wangeweza kupata bao tena na kujiweka katika nafasi nzuri.
Kipindi chote cha kwanza timu hizo zilitumia mfumo mmoja we
4-2-3-1 hivyo kuufanya mchezo uwe mgumu na unaofanana kwa kiasi fulani.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku wenyeji
waksihambulia zaidi na Lewandowski akafunga la pili katika dakika ya 49 wakati
wachezaji wa Madrid wakidhani ameotea kabla ya kuongeza la pili katika dakika
ya 54.
Baada ya hapo, mechi ilianza kuwa ya kibabe kila upande
ukicheza kindava na Wajerumani hao walionekana kuwa fiti zaidi. Lakini Lewandowski
akaweka rekodi na kufunga bao la nne kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 66.
Kutokana na kipigo hicho, Real Madrid inatakiwa kushinda mabao
3-0 nyumbani Santiago Bernabeu ili kutinga fainali itakayopigwa Mei jijini
London, England.













0 COMMENTS:
Post a Comment