April 26, 2013




Pamoja na sare Chelsea imejiweka katika nafasi nzuri ya kuingia nusu fainali ya michuano ya Kombe la Europa Cup baada ya kuichapa FC Basel ya Uswiss.

Chelsea ikiwa ugenini imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Waswiss hao ambao watalazimika kushinda Stamford Bridge jijini London, wiki ijayo.


Chelsea walipata bao lao katika dakika ya 12 baada ya Victor Moses kumalizia kona iliyoguswa na Branislav Ivanovic.

Bao hilo lilidumu hadi mapumziko lakini Basel walicharuka zaidi katika kipindi cha pili kutaka kupata bao la kusawazisha lakini haikuwa hivyo.



Baadaye Chelsea nusura wapate bao la pili baada ya shuti la Torres kugonga mwamba na kurudi uwanjani na mabeki wa Basel wakaondosha hatari.

Basel walipata bao la kusawazisha katika dakika ya 87 kupitia mkwaju wa penalti uliopigwa na Fabia Schar, hata hivyo penalti hiyo ilionekana kulalamikiwa kutokana na kuwa ya ‘magumashi’.

Wakati mechi inaoneka inakwenda ukingoni, David Luiz alifunga bao la pili katika dakika ya 90 kwa mpira wa adhabu.

Katika mechi nyingine ya nusu fainali, Benfica ilikuwa ugenini dhidi ya Fenerbahce ikiwa nyumbani nchini uturuki iliikaribisha Benfica ya Ureno.

Wenyeji walifanikiwa kupata bao katika dakika ya 71 kupitia kwa Egemen Korkmaz na Benfica wakaendelea kujitahidi kupata bao la ugenini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic