![]() |
| coastal union |
Vikosi vya Coastal Union ya Tanga na
Azam zitapambana Aprili 26 mwaka huu katika mechi ya Ligi Kuu Bara
itakayofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Awali mechi hiyo namba 168 ilikuwa
ichezwe Aprili 27 mwaka huu, lakini imerudishwa nyuma kwa siku moja ili kuipa
fursa Azam kujiandaa kwa mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya Kombe la
Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco.
Mechi hiyo itachezeshwa na Andrew
Shamba kutoka mkoani Pwani akisaidiwa na Abdallah Mkomwa (Pwani), Vicent Mlabu
(Morogoro) wakati mwamuzi wa mezani atakuwa Mohamed Mkono wa Tanga. Charles
Komba wa Dodoma ndiye atakayekuwa Kamishna wa mechi hiyo ya raundi ya 24.
Baada ya mechi ya Tanga, Azam
itarejea Dar es Salaam siku inayofuata tayari kwa safari ya kwenda Rabat
itakayofanyika Aprili 28 mwaka huu. Mechi hiyo itachezwa wikiendi ya Mei 3, 4
au 5 mwaka huu.
Keshokutwa (Aprili 24 mwaka huu)
kutakuwa na mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya African Lyon na JKT Ruvu
itakayochezwa Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.
Iwapo Azam itafanikiwa kusonga mbele
katika michuano ya Kombe la Shirikisho kutakuwa na marekebisho ya ratiba ya
ligi hiyo. Hiyo ni kutokana na raundi inayofuata ya Kombe la Shrikisho kuchezwa
wikiendi ya Mei 17, 18 na 19 mwaka huu ambapo bado haijajulikana Azam itaanzia
wapi (nyumbani au ugenini) iwapo itavuka.
Mechi nyingine za ligi hiyo ni
Aprili 25 (Ruvu Shooting vs Simba- Uwanja wa Taifa), na Aprili 28 (Simba vs
Polisi Morogoro- Uwanja wa Taifa).








0 COMMENTS:
Post a Comment