Soka mchezo wa aina yake, Sunderland ikiwa chini ya
kocha mwenye vituko, Paolo Di Canio imekumbana na kipigo cha mabao 6-1 kutoka
kwa Aston Villa.
Tayari Di Canio amewaomba radhi mashabiki wa
Seunderland kutokana na kipigo hicho alichokiita ni cha aibu.
Mshambuliaji Cristian Benteke
peke yake alipiga mabao matatu na kuilewesha Sunderland iliyopata bao pekee
kupitia kwa Danny Rose.
Mabao ya Aston Villa iliyokuwa
nyumbani yalifungwa hivi: Vlaar 31, Weimann 38, Benteke 55, 59, 72, Agbonlahor
88.
Kutokana na kipigo hicho,
Sunderland imebaki katika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 37 sawa na Aston Villa
na Newcastle kitu ambacho kimewapa hofu mashabiki.
Iwapo ingeshinda mchezo huo,
Sunderland ingekuwa imejiondoa kwenye wimbi la hofu ya kuteremka daraja.
0 COMMENTS:
Post a Comment