Mwamuzi mmoja nchini Russia amefungiwa maisha baada
ya kuamua kutoa kipigo kwa mchezaji wa timu aliyokuwa anaichezesha.
Adhabu hiyo imetolewa jana baada ya tukio hilo
limetokea la juzi katika mji wa Grozny wakati Amkar Perm ilipokuwa inaivaa Terek.
Mwamuzi huyo msaidizi Musa Kadyrov aliyekuwa na
kibendera, alikitupa ghafla na kuingia uwanjani na kuanza kumtandika mlinzi wa
Amkar, Ilya Krichmar mwenye miaka 18.
Kadyrov alimvamia mchezaji huyo baada ya mwamuzi
kupuliza kipenga cha kumaliza mpira.
“Alinisukuma nikiwa nimeanza kuelekea katika benchi
baada ya filimbi ya mwisho, baada ya kuanguka alianza kunipiga ngumi na mateke
na baadaye kuniburuza huku akiwa ameshika miguu yangu,” alisema Krichmar.
“Ajabu hata wachezaji wa timu pinzani waliungana na
mwamuzi huyo na kunishambulia mfulizo.
“Waliniumiza na damu zikaanza kutoka, lakini
wachezaji wenzangu walikuja na kunisaidia. Lakini ninamshukuru mmoja wa
wachezaji wa timu pinzani alinisaidia kutoka pale kwa kuwa tuliwahi kucheza
pamoja,” alisema beki huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment