Baada ya mwezi mzima wa mapumziko kutokana na kufanyiwa upasuaji, hatimaye
beki wa Yanga, Mbogo Ladslaus ameanza mazoezi na kikosi cha kwanza cha Yanga.
Mbogo
ameanza mazoezi na wachezaji wenzake wa Yanga jana kwenye Uwanja wa Bora
Kijitonyama, Dar es Salaam.
Wachezaji
wa Yanga walionekana wenye furaha kubwa kumuona Mbogo akiwa amerejea uwanjani.
Mwenyewe Mbogo
alionekana kuwa mwenye furaha na kabla ya kuanza mazoezi, alikutana na benchi
la ufundi lililoongozwa na Kocha Mkuu, Ernie Brandts raia wa Uholanzi na
kufanya majadiliano.
Baada ya
majadiliano hayo, Mbogo aliruhusiwa kuingia mazoezini na kufanya na kuendelea
na wenzake.
Daktari wa
Yanga, Nassor Matuzya alisema Mbogo atakuwa akifanya mazoezi ya taratimu hadi
hapo atakapokuwa safi.
Awali
ilielezwa kungekuwa na upasuaji wa pili katika shavu lake ili kuiweka sawa
ngozi, lakini baadaye Matuzya amesema wataangalia hali yake inaendelea vipi.
Imeelezwa uvimbe
alionao utakuwa unapungua taratibu na kwa muonekano wa leo, uvimbe huo wa
shavuni umepungua kiasi ikilinganishwa na awali.
Mbogo alifanyiwa upasuaji wa shavu lake ili kuondoa uvimbe, hali iliyomlazimu kukaa nje ya uwanja kwa kipindi hicho.







0 COMMENTS:
Post a Comment