April 19, 2013



 
Hatimaye beki wa Yanga, Mbogo Ladslaus anaanza mazoezi kesho na kikosi cha kwanza cha Yanga.

Mbogo alifanyiwa upasuaji wa shavu lake ili kuondoa uvimbe, hali iliyomlazimu kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki tatu sasa.

Akizungumza na Salehjembe leo jijini Dar, Mbogo alisema daktari wa Yanga, Nassor Matuzya amemueleza kuwa ataanza mazoezi kesho Jumamosi.


“Kweli dokta amesema nianze mazoezi asubuhi, nitaanza taratibu chini ya uangalizi wake,” alisema.

“Hakika nasikia faraja sana kwa kuwa nimekuwa nikitamani kurejea uwanjani lakini hali yangu ilinilazimisha kuwa na subira.”

Leo mchana kulipatikana kwa taarifa mpya kwamba ule upasuaji wa pili uliokuwa umepangwa kufanyika utalazimika kusubiri hadi hapo daktari atakapoangalia hali yake.

 “Dokta amesema wataangalia kwanza, kwamba kama kila kitu kinakwenda kama walivyotaka hata upasuaji wenyewe unaweza usifanyike.

“Inaweza ikachukua miezi miwili au zaidi ili kupata jibu la uhakika kuhusiana na nini kinatakiwa kufanyika,” alisema Mbogo.

Mbogo alifanyiwa upasuaji wa kwanza kuondoa uvimbe kwenye paji lake na ulikuwa wenye mafanikio makubwa.

Lakini baadaye ilielezwa kwamba lazima ufanyike upasuaji wa pili ili kuweka mambo vizuri.

Beki huyo alijiunga na Yanga msimu uliopita akitokea Toto African ya Mwanza ambayo sasa inahaha kubaki Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic