Baada ya msako mkali,
hatimaye polisi wa Marekani wamefanikiwa kumnasa Dzhokhar Tsarnaev, 19, mtuhumiwa wa pili wa ulipuaji
wa mabomu ya Houston Marathon.
Kijana huyo raia wa
Chechnya alikamatwa jana usiku baada ya kukutwa amejificha katika boti katika
eneo la Watertown nje kidogo ya Boston.
Tsarnaev alijificha
kwenye boti na kaka yake baadaye akafichua siri, polisi walipofika katika eneo
hilo akawa mbishi hivyo kufanya majibizano ya risasi yaanze kuanzia saa 1 usiku
hadi saa 2:30 usiku aliponyoosha mikono.
Hata hivyo ilielezwa
alinyoosha mikono baada ya kupigwa risasi mara mbili.
Baadaye alikamatwa damu
zikiwa zinamvuja mwili mzima na akakimbizwa hospitali kwa matibabu na taarifa
za awali zinaeleza alikuwa anatokwa damu nyingi sana.
Bado matibabu yanaendelea
na wananchi wlaijitokeza mitaani kushangilia kuhusiana na mlipuaji bomu huyo
ambaye pamoja na kaka yake aliishi Marekani tokea mwaka 2002.
Polisi walikuwa
wakimkimbiza kwa takribani siku mbili baada ya kaka yake aliyekuwa mtuhumiwa wa
kwanza kupigwa risasi na baadaye kufa akiwa hospitali.
Milipuko miwili karibu na
sehemu ya kumalizia mbio hizo za Boston Marathoni ulisababisha watu watatu
kupoteza maisha yao ikiwa ni pamoja na zaidi ya 100 kujeruhiwa wakiwemo 17
ambao walijeruhiwa vibaya.













0 COMMENTS:
Post a Comment