Mshambuliaji
wa TP Mazembe, Mtanzania, Mbwana Ally Samatta amekuwa gumzo kubwa katika mechi
ya kesho ya Ligi ya Mabingwa.
Mechi hiyo,
TP Mazembe itakuwa na kazi ya kuwavaa wenyeji wake Orlando Pirates, timu yenye
mashabiki wengi zaidi nchini humo.
Pirates na
Mazembe zimekutana zaidi ya mara mbili tokea mwaka 2000 na zimekuwa na upinzani
mkubwa.
![]() |
| Ndiaye.. |
Lakini
mashabiki wengi wa jiji la Johannesburg hasa Watanzania wamekuwa wakimzungumzia
Samatta.
Kwa mujibu
wa Mtanzania aitwaye John anayeishi jijini humo, amesema Samatta ndiye amekuwa
kivutio zaidi.
“Unajua
Pirates wanamtegemea Mzambia anaitwa Collins Mbesuma, lakini Wabongo na Wakongo
hapa wanamzungumzia Samatta.
“Hata
Mkongo mwenzao Tresor Mputu hawampi nafasi kubwa kama Samatta. Na hauwezi
kuamini tiketi zimekatwa kwa wingi sana hapa kwa ajili hiyo.
“Watanzania
wengi wanataka kwenda kumuona Samatta, maana baada ya kuwafunga Wamorocco mabao
mawili amekuwa gumzo sana hapa,” alisema John.
Tayari
Mazembe iko jijini Johannesburg na Kocha Mkuu, Lamine Ndiaye raia wa Senegal
amesema mechi hiyo itakuwa ngumu na yenye ushindani wa juu.
Lakini
akasisitiza amefurahishwa na wachezaji wake kuizoea haraka hali ya baridi huku
akionyesha matumaini kwamba wameizoea haraka hali ya hewa.
Baridi
imekuwa ikizidi kuwa kali nchini Afrika Kusini, awali Ndiaye alikuwa na hofu huenda
ingeathiri kikosi chake.









0 COMMENTS:
Post a Comment