Kocha Msaidizi
wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amekalia kuti kavu katika nafasi yake hiyo.
Tayari kuna
kikao kimefanyika kwa ajili ya kujadili kama Julio anaweza kubaki kuendelea
kuinoa Simba au la.
Taarifa za
uhakika ndani ya Simba zimeeleza kati ya vikao vilivyofanyika kujadili mambo
kadhaa na mustakabari wa Simba, imeelezwa Julio alijadiliwa.
“Kweli
tumemjadili Julio, inaonekana amekuwa akilalamikiwa karibu na kila upande,
wachezaji wakongwe, chipukizi na hata benchi la ufundi.
“Amekuwa
hana maelewano mazuri na karibu kila upande hali inayoonekana ni tatizo na
inapoteza utulivu ndani ya timu,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Hata hivyo
Julio amekuwa Mbogo na asiyependa kuzungumzia mustakabari wake.
Katika majadiliano
hayo, swali limekuwa ni kwamba Julio aondoke kabla ya msimu kwisha au baada.
Wako wanaounga
mkono aondoke kabla lakini wengine wanataka aachwe hadi Simba itakapomalizika
msimu kwa kuwa haina nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.
Hivi karibuni
Julio alinuniana na bosi wake, Patrick Liwig hali ilizorotesha utendaji wa kazi
wa benchi la ufundi.
Hata hivyo upande mwingine umeeleza kumekuwa na fitina zinazopikwa ili kumuondoa Julio katika nafasi yake kutokana na tabia yake ya kusema ukweli.
Julio amekuwa akiwaeleza wazi wachezaji wanaokosea hasa kuhusiana na suala la kutojituma mazoezini au kuitumikia timu kwammoja.







0 COMMENTS:
Post a Comment