MADRID V BETIS Pamoja na kwamba haina nafasi ya kutetea taji lake la La Liga, Madrid imeitandika Real Betis kwa mabao 3-1 huku mshambuliaji wake Mesut Ozil akifunga mabao mawili.
Bao moja lilifungwa na Karim Benzema na kuifanya Madrid izidi kujikita katika nafasi ya pili lakini ikaonekana ni kama mechi ya kujiandaa na Ligi ya Mabingwa hatua ya nusu fainali dhidi ya Borussia Dortmund.
BARCA V LEVANTE
Barcelona nayo imezidi kujikita kileleni na kujihakikishia kwamba lazima iwe bingwa La Liga baada ya kuichapa Levante kwa bao 1-0.
Barcelona nayo imezidi kujikita kileleni na kujihakikishia kwamba lazima iwe bingwa La Liga baada ya kuichapa Levante kwa bao 1-0.
Cesc
Fabregas aliyefunga bao hilo pekee huku ikionekana Barcelona si ile
iliyozoeleka hasa kutokana na kumkosa mshambuliaji wake nyota Lionel Messi.
Mechi
ngumu inafuatia kwa Barcelona ni ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya nusu
fainali dhidi ya Bayern Munich.










0 COMMENTS:
Post a Comment