April 21, 2013



 Wakati wa uhai wake msanii maarufu zaidi wa muziki wa taarabu, Fatuma binti Baraka alikuwa mpenzi mkubwa wa mchezo wa soka.

Binti Baraka maarufu kama Bi Kidude alifariki wiki iliyopita na kuzikwa mjini Zanzibar.


Bi Kidude ambaye anakadiriwa kufariki dunia akiwa na miaka 104, alikuwa akitaka kujua matokeo ya timu kadhaa ikiwemo timu ya vijana ya mtaani kwake.

Mjukuu wake aliyekuwa mlezi wa Bi Kidude, Omary Amiry amezungumza na Salehjembe kutoka mjini Zanzibar na kusema mara kadhaa liwahi kuwaahidi vijana wa mtaani kwake waliokuwa wanacheza soka kwamba angewanunulia jezi na mipira.

“Hata hivyo mara nyingi alisisitiza kwamba ni lazima washinde na mara nyingi walipotoka katika mechi aliwasimamisha na kutaka kujua matokeo.
“Kama alisikia wamefungwa aliwalaumu kwa kushindwa kuchangamka na kutaka mechi inayofuata washinde,” alisema Amiry.

“Hapa Raha leo kuna timu nyingi, lakini mara kadhaa walikuwa vijana wakiunganisha kombaini na kwenda kucheza. Hivyo Bi Kidude alikuwa akifuatilia sana matokeo.”


Bi Kidude amefariki dunia na kuacha rekodi ya msanii mkongwe zaidi nchini, Afrika na ikiwezekana dunia nzima aliyekuwa mkongwe huku akiendelea kufanya kazi yake ya usanii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic