Mkuu wa
Idara ya Uanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Primo Carvaro
ametua mjini Bujumbura, Burundi tayari kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro.
Carvaro
ametua mjini Bujumbura kimyakimya kusuluhisha mgogoro unaendelea katika
shirikisho la soka nchini humo.
Hata hivyo,
kumekuwa na hali ya kushangaza baada ya wanahabari kutojua lolote kuhusiana na
kuwasili kwake nchini humo.
Ramadhani
Kibuga, Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura ameiambia Salehjembe kuwa Carvaro
ameongozana na watu wengine ambao hawajajua ni akina nani.
“Imekuwa ni
kimyakimya ingawa kulikuwa na taarifa ya ujio wao, hivyo hatujui msafara wao
una watu wangapi,” alisema.
Inaelezwa
huenda ni ujumbe uleule uliotoka nchini siku chache na kufanya mahojiano na wagombea
kadhaa walioenguliwa kwenye uchaguzi wa TFF wakiwemo Jamal Malinzi na Michael
Wambura.
Wakati wakiwa
nchini, baada ya kuwahoji wagombea wote waliokuwa wameenguliwa, Carvaro
aliyekuwa ameongozana na Ashford Mamelodi walisema wanarejea Zurich, Uswiss
katika makao makuu ya Fifa ambako wataliwasilisha suala hilo.
Walisema baada
ya kuliwasilisha suala hilo, watakuwa na jibu kuhusiana na uchaguzi huo wa TFF
na Carvaro alisisitiza halitakuwa jambo gumu kama linavyoelezewa.








0 COMMENTS:
Post a Comment