Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig ametamba kikosi
chake kinaweza kushinda mechi mbili zilizobaki za dhidi Ligi Kuu Bara dhidi ya
Ruvu Shooting na Yanga huku akitumia kikosi kilichojaa vijana.
Liewig raia wa Ufaransa amesema ana imani kubwa na
wachezaji wake hao vijana na anaamini pointi sita zitapatikana.
“Kikosi change ndiyo hicho unachokijua, wala
hatuwezi kufanya mabadiliko hata kidogo. Tutacheza na Shooting na Yanga na
kufanya vizuri.
“Utaona mechi iliyopita dhidi ya Polisi, tulifanya
makosa kadhaa ambayo tunayafanyia kazi yasijirudie katika mechi ijayo na pia
ile dhidi ya Yanga.
“Wachezaji wangu wengi ni vijana, lakini
wanajifunza na wanaelewa. Hivyo sina hofu ya kutaka kuongeza mchezaji yoyote,”
alisema Liewig.
Kocha huyo alisema tayari amekuwa akizungumza na
wachezaji wake na kusisitiza kwamba hawana sababu ya kuwa na hofu na kama
ushindi dhidi ya Yanga ni kitu kinachowezekana.
0 COMMENTS:
Post a Comment