Azam FC imefanikiwa kutua salama salimini mjini
Rabat na kufikia katika katika Hoteli ya Golden Tulip tayari kuivaa AS Rabat Jumamosi
katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho.
Hata hivyo ikiwa njiani, ililazimika kununua vifaa
kwa ajili ya kupambana na baridi ya mjini Rabat.
Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd amesema wamefika
salama na kikosi chao kinaendelea vizuri.
“Tulipokuwa Dubai, katibu mkuu alinunua vifaa
maalum kwa ajili ya kupambana na baridi kwa kuwa hatujui kama hali ya hewa
inaweza kubadilika.
“Kesho tutakuwa na ratiba ya mazoezi na hatujajua
hali itakuwaje, lakini tunategemea mambo yatakuwa mazuri kwa kuwa wenyeji wetu
walitupokea vizuri sana.
“Tokea tumetua uwanja wa ndege na baadaye walileta
basi zuri kabisa ambalo tulisafiri nalo kutoka Casablanca hadi Morocco,”
alisema Jaffar.
Azam ina kazi kubwa ya kupambana na AS Rabat ambayo
katika mechi yao ya kwanza jijini Dar es Salaam walitoka sare ya bila
kufungana.
Hivyo Azam FC inatakiwa kushinda au sare ya aina
yoyote lakini lazima iwe ya mabao.
Kocha Stewart raia wa Uingereza amesema vijana wake
bado wana nafasi ya kufanya vizuri dhidi ya wenyeji wao hao na kusonga mbele.
PICHA KWA HISANI YA FACEBOOK YA AZAM FC
0 COMMENTS:
Post a Comment