Pamoja na taarifa za kurejea tena wa Zacharia Hans Pope kufanya kazi za Simba, lakini baadhi ya wajumbe walioshiriki mkutano wa usuluhishi wameonyesha kuwa na hofu na utekelezaji wa mambo kadhaa waliyokubaliana.
Rage na baadhi ya wajumbe wa kundi la Friends of Simba wamekubaliana
tena kufanya kazi pamoja katika mkutano ulioongozwa na Hans Pope ambaye pia
alikuwa amejiuzulu.
Lakini mjumbe mmoja amesema mara kadhaa, Rage amewahi kuwageuka, hivyo
wanataka kuona utekelezaji.
“Sisi hatukuwa na tatizo na utaona tulikubaliana mambo kadhaa ambayo
yanatakiwa kutekelezwa kwanza. Tutasubiri kuona utekelezaji umefanytika.
“Imewahi kutokea mara kadhaa, utekelezaji ukawa shida na chairman (Rage)
amekuwa hatekelezi mambo.
“Hivyo hatuwezi kusema kila kitu kimekamilika hadi utekelezaji
utakapofanyika lakini sasa tunarudi kufanya kazi za Simba pamoja.
“Kitu kizuri hata Hans Pope naye amekubali kurudi, hivyo tutakuwa pamoja
na tunachotaka kurekebisha mambo kadhaa na tumeomba tupewe nafasi,” alisema
mjumbe huyo.
Taarifa zinaeleza, baada ya kuona mambo magumu, Rage aliamua kuomba
kukutanishwa na maadui zake hao aliokuwa amewakoroga.
Hata hivyo nao waligawanyika kutokana na hofu ya kutoamini kama
watakachokubaliana kitakuwa kauli dhabiti.
Lakini Hans Pope aliwahakikishia atalisimamia na kuhakikisha mambo
yanakwenda vizuri na alisisitiza alikuwa ameahidiwa na Rage kwamba kila kitu
watakachokubaliana ndicho kutakwenda kama kilivyopangwa.
Simba sasa inawania nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi na inaonekana
haina uhakika wa kuipata.







0 COMMENTS:
Post a Comment