Zimebaki saa chache kabla
ya kiu ya Watanzania wapenda soka kukatwa.
Mechi ya Kombe la
Shirikisho kati ya Azam FC na FAR Rabat ya Morocco itapigwa kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar kuanzia saa 10 jioni.
Hata hivyo Azam FC
inapaswa kuwa makini na mambo haya matano kutoka kwa Wamorocco hao waliowahi
kuwa mabingwa.
Vichwa:
Wana sifa ya kuwa na
wachezaji wenye uwezo wa kupiga vichwa, maana yake Azam wanapaswa kuwa makini
katika hilo.
Krosi:
Wana mawinga wazuri na
wataalamu wa kuchonga krosi zenye macho, Azam wanabidi wazipe njia.
Kuchelewa:
Kwa kuwa wanacheza
ugenini, watafanya kila wanaloweza kupata bao la mapema na baada ya hapo
watapoteza muda na kushambulia mara chache kwa kushtukiza.
Kujilinda:
Wako ugenini, maana yake
watajilinda sana na hawatataka nyavu zao ziguswe ili wakamalize kazi nyumbani.
Kujiangusha:
Wajanja sana wanapoingia
katika eneo la hatari, wakiguswa tu wanajiangusha na kama refa ni wa mipango,
basi mmekwisha.







0 COMMENTS:
Post a Comment