FULL TIME:
Dk 90, Rabat wanazidi
kuupoza mpira, wakionyesha wazi wamepania kupata sare.
Dk 89, shuti kali la
Tchetche aliyelazimisha kupata nafasi kwa kuwahadaa mabeki linagonga mtambaa wa
panya na kutoka nje.
Dk 86, krosi ya Rabat
langoni mwa Azam inakosa mmaliziaji, ilikuwa hatari
Dk 83, Rabat wanaendelea
kupiga pasi fupi na kurudisha mpira nyuma wakionyesha sare inawatosha.
Dk 81, Azam wanafanya
shambulizi kali, lakini Bocco anashindwa kuunganisha krosi nzuri ya Sure Boy.
Dk 77, anatoka Mcha na
nafasi yake inachukuliwa na Gaudence Mwaikimba.
Dk 71, wanazidi kupiga
pasi fupi za kujiamini huku wakionekana hawana hofu hata kidogo.
Dk 69, Rabat wanaanza
kuupoza mpira kwa kupiga pasi fupi na kurudisha langoni mwao.
Dk 65, Tchetche anapiga
shuti kali linalopanguliwa na kipa Grouni, ilikuwa ni baada ya krosi ya Mao
kumparaza Bocco.
Dk 62, Waziri anapiga
shuti hafifu linalodakwa kilahisi, ilikuwa pasi nzuri ya Sure Boy baada ya Azam
kushambulia vizuri.
Dk 58, Azam wameamka
wanasukuma mashambulizi mengi kwa Rabat.
Dk 52, Azam wanafanya
shambulizi kali, shuti kali la Tchetche baada ya kupokea pasi ya Bocco linatoka
nje sentimeta chache.
HALF TIME:
Dk 35-43, Rabat
wanatawala mchezo kwa pasi fupifupi, wakionyesha kupoteza muda huku Azam FC
wakipoteza nafasi nyingi na kupoteza matumaini ya kupata bao kipindi cha
kwanza.
Dk 30, Al Fathi anaukosa
kidogo mpira, ilikuwa krosi nzuri ya Belakhdar, kama angeupata ingekuwa hatari
kwa Azam.
Dk 22, Mwadini anafanya
kazi ya ziada kupangua shuti la Al Bakkali na kuwa kona isiyo na madhara.
Dk 15 nafasi nzuri
wanatengeneza Azam FC, lakini pasi ya mwisho kutoka kwa Tchetche kwenda kwa
Sure Boy inakuwa fupi.
Dk 5 Azam wanapata pigo
baada ya beki wao wa kati Atudo kuumia, alikaa nje kwa takribani dk 7, akarudi
lakini nafasi yake imechukuliwa na Lukson Kakolaki.
Dk dk 2, kipa Groun wa
Rabat anafanya kazi ya ziada kupangua shuti kali la Bocco na kuwa kona ambayo
haina madhara.
AZAM FC
Mwadini, Mao, Waziri,
Mwantika, Atudo, Balou, Sure Boy, Mieno, Bocco, Tchetche na Mcha.
0 COMMENTS:
Post a Comment