Kiungo wa Mkenya, Victor Wanyama ameingia katika rekodi ya kuwa mmoja wa
wachezaji waliobeba ubingwa msimu huu.Wanyama na Celtic wamebeba ubingwa wa Ligi Kuu Scotland (SPL) baada ya kuichapa Inverness kwa mabao 4-1 katika mechi yao ya leo.
Wanyama ambaye amekuwa tegemeo katika kiungo cha timu hiyo alikuwa kati ya wachezaji waliocheza vizuri.
Hooper alifunga mabao mawili katika dakika ya 61 & 73,
mengine mawili yakafungwa na Ledley dakika ya 66 na Samaras, 88.
Wanyama amekuwa gumzo kati ya viungo wanaowania na klabu
kubwa mbalimbali kama Manchester United na Arsenal ingawa inaonekana ataendelea
kubaki Uskochi.








mkuu mbona sielewi wanyamba.wanyama niaje jooo au ni watu wawili ?
ReplyDelete