April 25, 2013




Kocha José Mourinho amekubali kurejea katika klabu yake ya zamani ya Chelsea.

Jarida maarufu la Ujerumani la Bild limesema lina uhakika Mourinho alimalizana na milionea Mrusi, Roman Abramovich.
Pamoja na kukubaliana na Abramovich, imeelezwa tajiri huyo amemuahidi Mourinho kuwa atamsajili mshambuliaji Radamel Falcao wa Atletico Madrid.
Pamoja na dau lake kuwa kubwa kwani Madrid wanahitaji euro milioni 60, lakini Abramovich amemueleza Mourinho kuwa atamsajili mshambuliaji huyo ili kumpa nafasi ya kufanya kazi kwa uhakika na anavyotaka.

Hata hivyo Mourinho ambaye inaelezwa kuwa ataondoka Madrid Julai, amekuwa hataki kulizungumzia suala hilo kwa madai bado ni muajiriwa wa Madrid na  nguvu nyingi kazielekeza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic