Pamoja na
kuwa mmoja wa mashabiki wanaojitokeza mara nyingi Yanga inapokuwa inacheza
Uwanja wa Taifa, Dar, muigizaji maarufu ameonekana kutojua lolote kuhusiana na
suala la kusimama dakika moja ya kutoa heshima.
Kawaida kunapokuwa
na mtu aliyepoteza maisha na anahusiana na soka au kiongozi wa serikali, mwamuzi
hupuliza filimbi na watu uwanja mzima husimama kwa dakika moja ya kuomba na
kuomboleza ikiwa ni sehemu ya heshima.
Lakini wakati
Yanga inaivaa Ruvu JKT wiki iliyopita, pamoja na mwamuzi Oden Mbaga kuliza
kipyenga kuashiria wakati wa kutoa heshima kwa marehemu Meja Jenerali Makame
Rashid aliyekuwa mwanamichezo, Ray aliendelea kukaa kitako.
Pamoja na
Ray, wasanii wengine wawili wa Bongo Movie, Chikoka na mwanadada Ketty
waliendelea kubaki katika siti zao.
Lakini
mchekeshaji, Steve Nyerere alionyesha kuchezwa na machale, akasimama na
kuungana na wengine kumpa heshima marehemu.
Achana na
Ray, mashabiki wengine wengi waliokuwa karibu na Ray walionekana kutolijua
hilo, wakabaki vitini kimya, kitu ambacho si picha nzuri kwa maana ya michezo
ni furaha na undugu pia.
Huenda Ray
hakujua hili, lakini wakati mwingine anaweza asirudie kwa kuwa yeye kama kioo
cha jamii anapaswa kuwa mfano.







0 COMMENTS:
Post a Comment