![]() |
| Amerudi... |
Kiungo wa zamani wa Bolton, Fabrice Muamba hatimaye amerudi
uwanjani na kucheza soka kwa mara ya kwanza baada ya kutofanya hivyo kwa
takribani mwaka sasa.
Muamba alilazimika kustaafu soka kutokana na ugonjwa wa moyo ambao
nusura uchukue uhai wake baada ya kuanguka uwanjani ghafla wakati wakiivaa
Tottenham Hotspurs katika mechi ya Kombe la FA.
Baada ya kuanguka, moyo wa Muamba ulisimama kufanya kazi kwa saa 78,
hali iliyozua hofu kubwa.
Lakini jana alirudi na kucheza mpira uwanjani tena lakini katika mechi
za kujitolea kwa ajili ya kutoa misaada maarufu kama ‘Five aside’.
Muamba alionekana ni mwenye afya njema na kushirikiana na wenzake vizuri
ingawa wapinzani wake walionekana kuwa na hofu kidogo.
Hata hivyo, Muamba alionekana kujiamini na kucheza soka vizuri huku
dhahiri akionyesha alikuwa na hamu sana na soka.










0 COMMENTS:
Post a Comment