Mabao matatu aliyofunga Robin van Persie katika mechi dhidi ya Aston Villa
yamemfanya aweke rekodi ya kuwa hat trick ya haraka zaidi tokea mwaka 2004.
Hat trick
hiyo ya van Persie ndani ya dakika 33 tu imemfanya kuweka rekodi mpya tokea ile
ya Mei 15, 2004 iliyowekwa na Mnigeria Yakubu Aiyegbeni wakati Portsmouth ilipokuwa
inaivaa Middlesbrough.
Katika
mechi hiyo ya Ligi Kuu England, Portsmouth ilishinda kwa mabao 5-1, Mnigeria huyo akipiga mabao hayo
matatu.
Pamoja na
rekodi hiyo, van Persie amejiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa tena tuzo ya
mchezaji bora wa mwaka, kwani amemzidi Suarez kwa bao moja katika listi ya
wafungaji lakini ameisaidia United kutwaa taji la 20 la Ligi Kuu England.








0 COMMENTS:
Post a Comment