Lile pambano kati ya makundi mawili maarufu ya Hip
hop nchini, Wanaume Family na Wanaume Halisi umemalizika.
Jibu ni kwamba, mashabiki lukuki waliojitokeza
kwenye Ukumbi wa Dar Live jijini Dar wamemchagua Nature na kundi lake la
Wauname Halisi.
Kazi haikuwa lahisi, kila upande ulipiga shoo yao
kwa awamu na Wanaume Family wakiongozwa na Temba, Chege, Bi Cheka, Dogo Asley
pia walikamua vilivyo.
Ukitazama shoo, Wanaume Family walifanya kazi nzuri
iliyokuwa na mpangilio bora zaidi. Lakini mashabiki waliendelea kushangilia na kuimba Nature huku wakionyesha vidole vitatu wakiwa na maana ya "tatu bila".
Lakini bado mashabiki wakachagua upande uliokuwa na
Nature, Inspektor Haroun, Dollo, KR, Dj Snox na wakongwe wengine. Wanaume
Halisi walionekana kung’ara zaidi katika nyimbo za zamani ambazo zilikuwa na
mashabiki wengi walioonekana kukumbuka enzi hizo.
Wakati Dj mkongwe, DJ JD alipopanda jukwaani na
kutangaza wa upande wa Nature waende upande huu na Wanaume Family upande ule,
upande uliokuwa wa Nature ndiyo ukawa na watu wengi zaidi.
Pambano hilo liliandaliwa na Global Publishers,
mashabiki walijitokeza kwa wingi licha ya mvua kunyesha mchana kutwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment