David Miliband (kulia),
ameachia ngazi nafasi ya makamu mwenyekiti.
Paolo di Canio ametangazwa kuwa kocha mpya wa Sunderland lakini Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyoo, David Miliband ametangaza kujiuzulu.
Milband amejiuzulu na kusema ameamua kufanya kazi za kusaidia jamii
jijini New York, Marekani lakini habari kutoka ndani ya klabu hiyo zimeeleza
amemkimbia di Canio raia wa Italia.
Mwaka 2005 huyo aliwa kusema yeye ana mwanasiasa wa kifashisti na wala
si mbaguzi wa rangi.
Miliband alisema: “Nawatakia Sunderland AFC kila la kheri katika mechi
zao saba zilizobakia, ninaamini watapambana na kufanya vizuri. Ilikuwa ni
sehemu nzuri kwangu lakini wakati umewadia.”
Pamoja na kujiuzulu kwa Miliband lakini mmiliki wa klabu hiyo, Ellis Short
anaonekana kumuamini di Canio kuwa ataiongoza Sunderland kukweka kuteremka
daraja.
Di Canio amechukua nafasi ya Martin O'neill aliyetimuliwa kutokana na
mwenendo mbaya wa timu yake katika Ligi Kuu England, mechi yake ya mwisho ni
pale ilipolala kwa bao 1-0 dhidi ya Man United.
0 COMMENTS:
Post a Comment