April 21, 2013




Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima ameonyesha hata Tanzania mambo yanawezekana, baada ya kumualika mwanaye aitwaye Ramuzy katika mazoezi ya timu yake.


Juzi, David Beckham aliwaalika wanaye watatu, Brooklyn, Cruz na Romeo katika mazoezi ya timu yake ya PSG jijini Paris na wakajumuika na nyota wengine kama Thiago na Zlatan Ibrahimovich.


Niyonzima alijumuika na Ramuzy katika mazoezi hayo ya Yanga na Ramuzy alikuwa akijaribu kuonyesha ujuzi wake ikiwa ni pamoja na kukimbia na wachezaji wa Yanga.



Kocha wa Yanga, Ernie Brandts naye alimkaribisha Ramuzy anayekadiriwa kuwa na miaka minne na kutaka kujua uwezo wake wa kukipiga.

Wachezaji wote wa Yanga walimfurahia Ramuzy na mara nyingi alionekana kucheza na kucheka na Athumani Iddi ‘Chuji’, Godfrey Taita na mkongwe, Shadrack Nsajigwa.

Pamoja na kuwa na idadi kubwa ya watu pamoja na wachezaji, mtoto huyo aliyekuwa amepiga uzi wa Yanga alionekana kutojali na kuendelea na hamsini zake.

Niyonzima ni raia wa Rwanda ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika misimu miwili ambayo amekipiga Jangwani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic