Mambo yanazidi kuwa magumu kwa mshambuliaji wa Liverpool, Luiz Suarez
baada ya Shirikisho la Soka England (FA) kutangaza kumfungia mechi 10.
Kitendo cha kufungiwa mechi 10, maana yake Suarez ametoa nafasi ya
mshambuliaji wa Manchester United, Robin van Persie kuwa mfungaji bora.
Pamoja na nafasi ya kuwa mfungaji bora kutoweka, lakini inaonekana hana
nafasi tena ya kuwa mchezaji bora ambayo alikuwa anachuana zaidi na van Persie
na Gareth Bale.
Van Persie anaongoza kwa ufungaji akiwa na mabao 24, zaidi ya bao moja
kwa Suarez mwenye mabao 23.
Suarez alikuwa anaongoza, lakini mabao matatu ya van Persie katika mechi
dhidi ya Aston Villa imemfanya aongoze kwa bao hilo moja na kwa kuwa ataendelea
kucheza ana nafasi ya kuongeza tena wakati Suarez hatacheza tena hadi mwisho wa
msimu.
Liverpool na Man United, zote zimebakiza mechi tano za ligi, maana yake
van Persie ana nafasi ya kuendelea kuongeza mabao.
Adhabu hiyo ni ya pili kwa Suarez, kwani tayari amepigwa faini na Liverpool kutokana na
kitendo cha kumng’ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic.
Kabla ya kutua England wakati anaichezea Ajax, Suarez aliwahi kumng’ata
mchezaji wa timu pinzani, hali ambayo imekuwa ikiwashangaza wengi kutokana na
tabia za ajabu za mshambuliaji huyo mbaguzi wa rangi.









0 COMMENTS:
Post a Comment