Wachezaji
kadhaa maarufu wa Brazil amkiwemo Ronaldo, Bebeto walionekana kwa mara nyingine
wakiwa uwanjani wakati wa ufunguzi wa Uwanja wa Maracana.
Uzinduzi
wa uwanja huo ni baada ya ukarabati kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia na
Michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani nchini humo.
Mechi
hiyo ilikuwa ni kati ya marafiki wa Ronaldo na wale wa Bebeto na ilikuwa ni
burudani kutokana na wachezaji wengi kuwa na maumbo makubwa lakini wakajitahidi
kuonyesha makali.
Wakali
hao walicheza mechi na kutoa burudani ya kutosha lakini nje ya uwanja huo
kulikuwa na vita kati ya Polisi na waandamanaji waliokuwa wakipinga
ubinafsishwaji wa uwanja huo kwa madai serikali itapoteza mapato.
Rais
wa Brazil, Dilma Rousseff na Rais wa zamani wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da
Silva walikuwa kati ya watu 30,000 waliojitokeza katika uzinduzi huo.










0 COMMENTS:
Post a Comment