Katika soka hakukosi vituko, katika mechi ya Ligi
Kuu Bara kati ya Ruvu JKT na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, jana,
kumeibuka TV mpya inayoitwa Ukombozi.
Ukombozi TV inaongozwa na mashabiki wa Yanga na
vifaa vyake ni vya aina yake, halafu haionekani eneo lolote zaidi ya Uwanja wa
Taifa.
Wanaoonekana kwenye Ukombozi TV ni mtangazaji na
cameraman tu, lakini mashabiki hawana hiyana na wanakubali kuhojiwa.
Raha ya hiyo TV, inatangaza mechi na matukio ya
Yanga tu. Hebu jionee mwenye namna watu wa Ukombozi TV wakiwa kazini.







0 COMMENTS:
Post a Comment