Mtukutu
na mbaguzi maarufu wa rangi, mshambuliaji Luis Suarez we Liverpool ameomba radhi
kutokana na kitendo chake cha kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic
katika mechi yao ya Ligi Kuu England jana.
Katika
mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2, Suarez akiwa shujaa, lakini
akaonyesha kitendo cha ajabu kwa kumg’ata mkononi beki huyo wakati wakiwania
mpira.
Pamoja
na Suarez kuomba radhi, lakini imegundulika ndiyo tabia yake na jana haikuwa
mara ya kwanza kumng’ata mtu uwanjani.
Mwaka
2010 wakati akiicheea Ajax ya Uholanzi, alimng’ata mchezaji wa PSV Eindhoven, Otman
Bakkal hadi alama za damu zikajitokeza katika jezi.
Baadhi
ya mitandao imeanza kupendekeza kuanzishwa kwa sheria mpya ikiwa ni pamoja na
kuwapa adhabu watu kama Suarez kucheza wakiwa wamezibwa midomo yao.
Baadhi
ya picha zimeonyesha Suarez akiwa amezibwa kama mbwa wakorofi ili kuepusha
wasiume watu.
Mitandao
mingine imetania kwamba Suarez alikuwa ni mwenye njaa ndiyo maana kashindwa
kujizuia na alipomuona Ivanovic alifikiri ameona bugger, hivyo akajisevia na
kung’ata kwa juhudi kubwa.
Suarez
haishi vituko kwani miezi kadhaa iliyopita alikumbana na adhabu ya faini ya
pauni 40,000 na kusimamishwa kucheza mechi nane za Premiership baada ya
kumfanyia vitendo vya kibaguzi beki wa Manchester United, Patrice Evra raia wa
Ufaransa.
Taarifa
nyingine zilieleza kwamba Ivanovic ambaye huaminika ni mtaratibu, alizungumza
na maofisa wa polisi wa Merseyside mara tu baada ya mechi, lakini hakutaka
kufungua mashitaka au kwenda nje ya sheria za soka kuhusiana na suala hilo.












0 COMMENTS:
Post a Comment