| Julio na Liewig.. |
Uongozi wa Simba pamoja na kamati ya ufundi ya
klabu hiyo umekaa na kujadili suala la wachezaji wapya.
Kikao hicho cha siri kimefanyika jijini Dar es
Salaam na wachezaji kadhaa kutoka katika klabu mbalimbali wanaoonekana wanafaa
wamewajadili.
Kamati ya ufundi ya Simba, imechukua mapendekezo ya
kocha pamoja na mapendekezo yake na kuyajumuisha na kujadili pamoja na uongozi.
“Kilichojadiliwa ni wachezaji wapi wanaotufaa kwa
ajili ya msimu ujao lakini tumeangalia mapengo, hasa nafasi zilizosumbua msimu
huu,” kilieleza chanzo.
“Kidogo Simba kuna tatizo la fedha lakini kuanza
kujadili mambo mapema ni suala la msingi halafu fedha zitatafutwa.”
Kati ya nafasi zilizokuwa tatizo ni beki wa kati,
washambuliaji wawili namba tisa na kumi na hasa baada ya Mzambia Felix Sunzu
kutofanya vizuri kwa takribani misimu miwili sasa.
Kocha Mfaransa, Patrick Liewig pamoja na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amekuwa akipendekeza
kutumia vijana zaidi ingawa wazo hilo hakuwa amelianzisha yeye.
Uongozi wa Simba ulimuondoa Mserbia, Milovan
Cirkovic na kumchukua Liewig lakini inaonekana mambo yalivyo ni ‘Leo, afadhari
ya jana’.







0 COMMENTS:
Post a Comment