Uongozi
wa Liverpool kupitia Ian Ayre umesisitiza utabaki upande wa mshambuliaji wao,
Luis Suarez pamoja na kwamba alimuuma beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic.
Lakini
imeelezwa pamoja na maneno hayo matamu ya Liverpool, kimyakimya imempiga faini
Suarez kutokana na kitendo hicho walichokiita si cha kiungwana.
Suarez
alimuuma Ivanovic wakati wakigombea mpira katika mechi ya Ligi Kuu England
dhidi ya Chelsea ambayo ilimalizika kwa sare ya mabo 2-2, yeye akisababishwa
moja walilofungwa Liverpool lakini akapoza machungu kwa kufunga la kusawazisha.
Suarez analipwa mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki na faini aliyopigwa itakuwa kati ya zile kubwa zilizowahi kutokea ndani ya misimu mitatu ya EPL.
Taarifa
kutoka ndani ya Liverpool zinaeleza, Suarez amepigwa faini kati ya pauni 200,000
na 400,000 ambao ni mshahara wake kati
ya wiki mbili na tatu na utapelekwa katika vikundi vya kusaidia familia zenye
matatizo.
Imeelezwa
lengo la Liverpool kufanya mambo kwa siri ni kujaribu kupoza adhabu kutoka FA
ambayo inaaminika lazima itamuadhibu.
Hata
hivyo Ayre amesisitiza kwamba wataendelea kufanya kila linalowezekana
kubadilisha tabia ya Suarez.
Lakini
bado Liverpool imesisitiza, Suarez mwenye mtoto mmoja hatauzwa na ataendelea
kubaki klabuni hapo.









0 COMMENTS:
Post a Comment