Muda
mchache baada ya kupigwa faini na klabu ya Liverpool, mshambuliaji Luis Suarez
ameziti kuingia matatani.
Kampuni
ya vifaa vya michezo ya Adidas ambayo
hutangazwa pia na Suarez imesema inalichukulia suala hilo kama kitu
kikubwa.
Tayari
imeshatoa taarifa ya kutofurahishwa na Suarez kumng’ata beki wa Chelsea, Branislav
Ivanovic katika mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Anfield,
Liverpool.
“Tutamkumbusha
Suarez kiwango tulichojiwekea cha watu tunaotaka kufanya nao kazi na nini
tunakuwa tunategemea kutoka kwao,” ilieleza taarifa kutoka Adidas na kufafanua
zaidi.
“Tunafurahishwa
na namna Liverpool wanavyolipeleka suala hilo, tunaamini wanakwenda vizuri.
Luis amekubali alichokifanya si sahihi na tunaamini mambo yataenda vizuri.”
Kitendo
hicho cha Suarez kumng’ata Branislav
Ivanovic kimechukua nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari dunia nzima na
kufunika kabisa alichokifanya kusawazisha bao katika dakika za nyongeza na
kufanya matokeo yawe sare ya mabao 2-2.









0 COMMENTS:
Post a Comment